LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA LEO NI JUVENTUS VS REAL MADRID

Na Edo Daniel Chibo

Hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Barani ulaya inaendelea leo usiku kuanzia
majira ya saa nne kasorobo kwa saa za Afrika mashariki.

Juventus ambao wametawazwa mabingwa wa Italia wiki iliyopita kwa mara ya nne mfululizo itakua nyumbani katika dimba la Juventus jijini Turin kuwaalika Mabingwa mara 10 na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Klabu ya Real Madrid toka Spain.

Real Madrid wakiwa na mchezaji bora kabisa duniani hivi sasa imeshasafiri mpaka jijini Turin tayari kwa mchezo huo wa leo ambao utachezeshwa na Mwamuzi Martin Atkinson wa Uingereza.

Real Madrid watamkosa mchezaji wao karim Benzema ambaye ameshaifungia Madrid bao 22 msimu huu ambaye ameshindwa kurudi katika hali yake ya kawaida licha ya kuanza mazoezi mepesi hivyo kumpa nafasi Javier Hernandez “Chicharito” kucheza katika mechi ya leo kama kocha ataamua kumpanga.

Kwa upande wa Juventus wao hawana cha kupoteza kwani nguvu zao zote sasa wanazipeleka katika michuano hiyo huku ikitegemewa kuwaanzisha Andrea Pirlo na
Giorgio Chiellini ambao walipigwa benchi katika mechi iliyopita katika ligi dhidi ya Sampdoria.

UNAPASWA KUYAJUA HAYA KUELEKEA PAMBANO HILO


  •  Real Madrid ndiyo klabu ya kwanza kushiriki fainali za klabu bingwa barani Ulaya ikishiriki mara 13 na kufanikiwa kulibeba mara 10 na mechi ya leo ni kama marudio ya mechi ya fainali katika kombe hilo mwaka 1998 katika jiji la Amsterdam ambapo Real Madrid walishinda kwa bao 1-0 goli la Predrag Mijatovic .
  • Katika mechi saba zilizopita ambazo Real Madrid walisafiri kuzikabili timu za Italia hawakufanikiwa kupata ushindi.
  •  Juventus hawajafungwa katika mechi 12 zilizopita katika michuano ya Ulaya wakicheza nyumbani.
  • Real Madrid wamefikisha dakika 444 bila kuruhusu goli katika michuano ya mwaka huu ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wakicheza ugenini.

No comments

Powered by Blogger.