KABLA HUJALALA KAMATA HIZI AMBAZO ZIMEJITOKEZA LEO KATIKA USAJILI ULAYA


Manchester United na Arsenal wako katika vita kali ya kumwania mshambuliaji wa Real Madrid Mfaransa  Karim Benzema mwenye miaka 27 ambaye thamani yale ni paundi milioni 40m.
(Guardian)

Kocha wa Man United Louis van Gaal ametenga pia fungu la kumnasa beki wa pembeni wa Barcelona Dani Alves mwenye miaka 32,
(Daily Telegraph)

Kiungo wa Juventus Paul Pogba mwenye miaka 22 amekanusha uvumi wa yeye kutaka kurudi England hasa katika klabu ya Manchester United kwakua ndoto yake hivi sasa ni kujiunga na timu za Spain hasa  Barcelona na  Real Madrid.
(L'Equipe - in French)

Anayetarajiwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid Rafael Benitez amemwambia Rais wa klabu hiyo ya Real Madrid Florentino Perez mipango yake ni kuitengeneza timu kwa kumtumia mshambuliaji Gareth Bale mwenye miaka 25 kama atapewa nafasi ya kuifundisha klabu hiyo
(Daily Mirror)

Klabu ya Valencia imewaambia Manchester United wanatakiwa kulipa kiasi kisichopungua paundi milioni 35 kama wanataka kumsajili mlinzi wa timu hiyo Nicolas Otamendi mwenye miaka 27,
(Daily Star)

Mshambuliaji wa Chelsea na mchezaji bora wa ligi kuu ya England Eden Hazard mwenye miaka 24 amesema anafurahia maisha ndani ya Chelsea na angependa kukaa hapo kwa muongo mmoja zaidi.
Hazard ameshinda ubingwa wa Ligi kuu, Kombe la Ligi (Capital one) na kombe la Europa tangu alipojiunga na Chelsea mwaka 2012.
(London Evening Standard)

Kuna kila dalili kuwa Liverpool watamsajili mshambuliaji wa Astoni Villa mwenye miaka 24 Christian Benteke na wanasubiri kupeleka dau lao baada ya mechi ya fainali kombe la FA kati ya Arsenal na Aston Villa Jumamosi
(The Times )

Wachezaji wa Liverpool wameaandaa safari ya siku tatu "kula bata" Dubai mara baada ya kulambishwa bao 6-1 na Stoke City katika mechi ya mwisho katika ligi safari hiyo ikiwa ni maalumu kwajili ya kumuaga Steven Gerard
(Daily Mail)

Winga wa Arsenal Theo Walcott mwenye miaka 26, ataanza mazungumzo na klabu yake hiyo wiki ijayo kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi cha Arsenal 
(Daily Mirror)

Baada ya kukataliwa dau la paundi milioni 5 mwezi Januari kwaajili ya kumsajili kiungo mdachi Jordy Clasie, Southampton wanatakiwa kulipa paundi milioni 12.7 kama bado wana mpango wa kumsajili kiungo huyo mwenye miaka 23 toka Feyenoord. (Daily Star)

Newcastle United wanatarajia kumtangaza kocha mpya wa timu hiyo ndani ya wiki chache zijazo na wanaopewa nafasi ni pamoja na meneja wa zamani wa England Steve McClaren, Kocha wa zamani wa Lyon Remi Garde na.kocha wa zamani wa Swansea Michael Laudrup
(Guardian)

NOTE: HABARI HIZI ZOTE NI KWA MUJIBU WA MAGAZETI NA MITANDAO MBALI MBALI.

KWA LEO NI HAYO TU TUKUTANE TENA KESHO
~ EDO DC

No comments

Powered by Blogger.