INSIDE UNITED - TETESI ZA USAJILI WA MANCHESTER UNITED
Katika INSIDE UNITED leo tutaangalia tetesi za usajili katika klabu ya Manchester United habari ambazo zimetawala katika mitandao mbalimbali kuhusisha Manchester United
Habari zimetapakaa kwamba winga wa Benfica na timu ya taifa ya Argentina Nicolas Gaitan ameingia makubaliano na Manchester United na kiasi cha paundi milion 21 zimeshatengwa kwaajili ya usajili wake huku ikitegemewa kutangazwa Rasmi Ijumaa japokua maahabiki wengi wa Man United wamepondea usajili huo na kusema kuwa United inahitaji beki wa katikati na sio winga.
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane amesema hafikirii kuihama klabu hiyo kwani anaamini mafanikio yake atayapata akiwa na Spurs na hii ni alama tosha kuwa hana mpango wa kuhamia Man United baada ya kuhusishwa
Wakala wa Beki wa Valencia Nicolas Otamendi amesema mteja wake anataka kuondoka Valencia baada ya kusikia anatakiwa na Man United.
Kocha wa Bayern Munich Pep Guadiola anaamini kiungo wake Bastan Schweinsteiger ambaye amekua akiwindwa na Manchester United atabaki klabuni hapo.
Bosi wa Borussia Dortmund Michael Zorc anatarajia beki wa timu hiyo Mats Hummels hawezi kwenda Manchester United kwakua bado wanampenda na kuthamini mchango wake.
Kwa Leo tuishie hapa kwa habari zingine zinaihusu Manchester United tukutane kesho
No comments