DANNY WELBECK KUIKOSA FAINALI YA FA JUMAMOSI
Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck ataikosa mechi ya fainali ya kombe la FA baina ya timu yake Arsenal na Aston Villa itakayopigwa siku ya Jumapili katika dimba la Wembley kutokana na maumivu ya goti.
Welbeck alifunga goli la Ushindi katika mechi ya robo fainali dhidi ya timu yake ya zamani ya Manchester United katika dimba la Old Trafford na kukosekana kwake katika fainali kutawapa nafasi washambuliaji wengine wa timu hiyo Alexis Sanchez, Theo Walcot aliye katika kiwango bora hivi sasa na Olivier Giroud kuibeba safu ya ushambuliaji ya Arsenal
Amekosa mechi 5 zilizopita katika kukamilisha msimu ulioisha hivi karibuni ambapo Arsenal walifanikiwa kushika nafasi ya 3 na sasa atakosa pia mechi mbili za timu yake ya taifa ya England dhidi ya Slovenia na Jamhuri ya Ireland.
TOFAUTI YA WELBECK NA WASHAMBULIAJI WENGINE ARSENAL 2014/2015
WELBECK
Amwcheza mechi 27Amefunga magoli 4
Pasi za magoli 3
WALCOT
Amwcheza mechi 14Amefunga magoli 5
Pasi za magoli 0
GIROUD
Amwcheza mechi 27Amefunga magoli 14
Pasi za magoli 3
SANCHEZ
Amwcheza mechi 35Amefunga magoli 16
Pasi za magoli 8
No comments