ARSENAL YAIBANA MAN UNITED OLD TRAFFORD


Arsenal imezidi kujisogeza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini England baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Manchester United 

Pambano hilo lililopigwa katika uwanja wa Old Trafford lilikua zaidi kutafuta timu ipi itafanikiwa kushika nafasi ya tatu katika msimamo.

Man United ilitangulia kupata bao la kwanza likifingwa na Kiungo Ander Herrera akitumia vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Ashley Young likiwa ni goli la kwanza Arsenal wanafungwa kipindi cha kwanza tangu mwaka mpya walipofungwa na Southampton.

Arsenal wakasawazisha kipindi cha pili wakitumia makosa ya beki wa United Tayler Blacket aliyejifunga wakati akijaribu kuokoa mpira.

Radamel Falcao ambaye alianza katika mchezo huo alitolewa dakika za mwanzo za kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Robin Van perse huku Falcao akiwaaga mashabiki wa United kwa kuwapungia mkono mashabiki kama ishara ya kuwaaga katika mechi ambayo ni ya mwisho nyumbani kwa United msimu huu.

MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA BAADA YA MCHEZO HUO.


- Ander Herrera amefunga magoli 6 katika mashuti 7 aliyopiga kulenga goli la upinzani msimu huu.

- Goli la kujifunga la Tyler Blacket limemfanya kuwa mchezaji wa pili kujifunga katika mechi kati ya United na Arsenal mchezaji wa kwanza akiwa Gary Pallister katika sare ya bao 2-2 mwaka 1994.

- Arsenal wamefungwa goli la kwanza kipindi cha kwanza likiwa ndo goli la kwanza kufungwa kipindi cha kwanza tangu siku ya mwaka mpya walipofungwa Southampton

- Arsenal walishindwa kupiga shuti lolote golini kipindi cha kwanza hii ni mara ya kwanza kufanya hivyo katika ligi tangu mwaka 2004.

- Ilikua mechi ya kwanza kwa Victor Valdes katika mashindano Tangu mwezi Machi 2014 alipoumia akiitumikia Barcelona.

No comments

Powered by Blogger.