MAN CITY YAIFUMUA SWANSEA NA KUJIHAKIKISHIA NAFASI YA PILI
Pambano la ligi kuu nchini England baina ya Manchester City na Wenyeji Swansea City limemalizika kwa Man City kuibuka nabushindi wa bao 4-2.
Pambano hilo lililopigwa katika dimba la Liberty nyumbani kwa Swansea City lilishuhudia Yaya Toure akiwa ndo nahodha kukiongoza kikosi cha Man City baaada ya Vicent Kompany kuanzia benchi.
Yaya Toure alitangulia kuipatia Man City bao la kwanza kisha James Milner akaongeza la pili kabla ya Gyfil Sidgusson hajafunga bao la kwanza kwa Swansea City na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Man City wakiwa mbele kwa bao 2-1.
Bafetimbi Gomis alifunga bao la kusawazisha kwa Swansea na kufanya mchezo kuonekana unaweza kuisha kwa matokeo ya sare hiyo ya bao 2-2 lakini Yaya Toure na Wilfried Bony wakaongeza bao moja kila mmoja na kufanya mchezo huo kuisha kwa bao 4-2.
Kwa matokeo hayo Man City wamefikisha pointi 76 katika nafasi ya pili pointi ambazo zinaweza kufikiwa na Arsenal pekee
▪▪▪▪▪▪▪○○○○○○○○○○○○○○▪▪▪▪▪▪▪▪▪
No comments