JE HASSAN KESSY au JUMA ABDUL NI MBADALA SAHIHI WA NSAJIGWA?



Hassan Kessy Ramadhan si jina kubwa sana lakini ni miongoni mwa majina machache yaliyotawala sana vichwa vya wapenda soka wa Tanzania msimu huu. Kijana huyu anayekipiga katika klabu ya wekundu wa msimbazi Simba alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili wa Januari akitokea kwa wakata miwa wa Turiani Mtibwa sugar.

     Kessy amejizolea umaarufu mkubwa kwa muda mchache alioichezea Simba na hii inatokana na kiwango bora alichokionyesha licha ya umbo lake la kawaida.

Ni mchezaji mwenye pumzi ya kutosha na ni mzuri wa kukaba na kuipandisha timu mbele na ni mpishi mzuri wa magoli sababu ambayo imepelekea mashabiki kumfananisha na nyota wa Barcelona Dani Alves.

 Tofauti na wachezaji wengi wa hapa Tanzania Kessy anajiamini sana akiwa uwanjani na hata nje ya uwanja hakika kijana huyu ameitendea haki jezi yake namba 4 ambayo ameichagua kuivaa jezi ambayo imewahi kuvaliwa na wakali wengi waliopitia katika klabu ya Simba akiwemo mlinzi Victor Costa Nampoka.

     Achana na Kessy sasa hamia makutano ya mtaa wa  Jangwani na Twiga Jijini Dar es Salaam kwa mabingwa wapya wa Ligi kuu Yanga SC kuna kijana  anaitwa Juma Abdul huyu naye kama Kessy ameibuka na kuwa mmoja wa mabeki bora ndani ya uzi wa kijani na njano yaani Yanga.

Juma Abdul anaimarika kadri siku zinavyosogea hasa kwa pasizake maridadi, kublock mipira na pia kupandisha mashambulizi akiwa ni msaada mkubwa kwa Saimon Msuva ambaye ameng'ara vilivyo upande ule wa kulia wa yanga.

Asilimia kubwa ya magoli ya Yanga yanatengenezwa upande huo  na pia ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti na krosi. Ukiachana na michezo ya ligi kuu Juma Abdul ameonyesha kiwango maridhawa katika mechi ngumu za kimataifa mwaka huu!

   Hakika vijana hawa wamejitahidi sana na kuonyesha kuwa wanaweza kuja si kuziba tu ile nafasi ya Nsajigwa katika timu ya taifa bali kuifikisha mbali zaidi timu yetu ya Taifa ya Tanzania na hususani vilabu vyao.

Asanteni
By Vedasto Mfilinge (Member: Wapenda Soka Tanzania)
 0659812805

2 comments:

  1. Bila shaka kwa hawa upo sahihi sana ila tu tatizovi vilabu vyetuhaviwatendeivijana haki mfano lile sakata la SihaviwatendeisKessy Kessy na kwa muono wangu kama Simba wangeshinda zile mechi mbili (vs Stand Shinyanga na Vs Mbeya City Sokoine) sidhani sana kama wangeendelea kuhangaika na Kessy na ndo ungekuwa mwanzo wa kupotea ila vijana kweli wana kipaji na wanakitendea haki.

    ReplyDelete
  2. Bila shaka kwa hawa upo sahihi sana ila tu tatizovi vilabu vyetuhaviwatendeivijana haki mfano lile sakata la SihaviwatendeisKessy Kessy na kwa muono wangu kama Simba wangeshinda zile mechi mbili (vs Stand Shinyanga na Vs Mbeya City Sokoine) sidhani sana kama wangeendelea kuhangaika na Kessy na ndo ungekuwa mwanzo wa kupotea ila vijana kweli wana kipaji na wanakitendea haki.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.