WACHEZAJI WA ENGLAND WANAHARIBIWA NA VYOMBO VYA HABARI


Na Zahir Bilal
Wakati fulani mpiganaji maarufu wa sanaa za mapigano wa nchini China marehemu Bruce Lee aliwahi kusema "Always be yourself,express yourself,have faith on yourself and do not go out and look for a successful personality and duplicate it". (Daima jiamini na ufanye mambo yako usimtafute aliyefanikiwa ili uje kumuiga)

Hili ndio kosa wanalolifanya Waingereza hasa katika miaka ya hivi karibuni kwa vijana wao ambao wanachipukia katika soka,mzimu huu wa kufananisha unaua vipaji vya wachezaji wao wa ndani matokeo yake wanabweteka na baada ya miaka kadhaa kuonekana wa kawaida mno ukiachilia mbali viashiria vizuri vya vipaji vyao mwanzoni kabisa mwa maisha yao ya soka.

Usishangae kuona kijana mwingereza mwenye umri kuanzia miaka 17 had 21 akifananishwa na Xavi,Iniesta au Henry huu umekua kama utamaduni wa vyombo vyao vya habari wanasahau katika umri kama huo mchezaji yoyote anatakiwa aangaliwe kwa ukaribu zaidi na kuna mawili kumtengeneza awe bora au kumuharibu kabisa na nionavyo hawa waliokuwa watawala wetu wamechukua njia hiyo ya pili na hawajajifunza bado hapa wangeenda kuumuuliza yule mzee aliyeacha historia pale Uingereza (Ferguson) aliwatunzia vipi wale vijana wake wa  1992 waliokuja kujitengenezea historia ya kwao wenyewe baadae.

Sitaki kuzungumzia kizazi chao cha dhahabu cha kina Steven Gerrard, Frank Lampard,Ashley Cole na wengine wengi tu pamoja na kutokufanikiwa kwao kwenye timu ya taifa lakini hawakufanya vibaya katika vilabu vyao walivyochezea na wanavyochezea mpaka sasa.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kizazi hicho cha kina David Beckam na hiki cha kina Andres Townsend, Theo Walcott, Micah Richards,Adam Johnson, Jack Rodwell....
Kuna wakati vyombo vya habari vya Uingereza vilitaka tuamini Theo Walcott angelivaa viatu vya gwiji Thiery Henry akiwa bado kijana mdogo kabsa walisahau soka sio kipaji tu kuna vitu vingi vya kujifunza hasa kwa vijana kama Theo,yale mabao ya Henry yaliyowaacha watangazaji na watazamaji midomo wazi haikua kazi ya usiku mmoja.

Hawakuishia hapo tu Wenger alikua na silaha nyingine yenye kipaji maridhawa aliyoipeleka Bolton kwa mkopo na alipomrejesha alifanya mambo makubwa si mwengine huyu alikua ni Jack Wilshere ambaye alitamba mbele ya viungo hatari duniani Xavi na Iniesta kwenye ubora wao katika dimba la Emirates alipiga pasi,alikokota mali atakavyo,alipora mipira na kuisogeza timu,siku hizi anacheza nusu msimu nusu iliyobaki anaishia kwenye chumba cha matibabu na ndio kwanza ana miaka 23.

Sasa hivi waingereza wamepata pa kusemea baada ya kuishi chini ya kivuli cha Gareth Bale sasa wana Harry Kane huyu anawafanya wachambuzi wa kiingereza watune na kutamba huu ndio msimu wake wa kwanza kucheza karibu mechi zote baada ya kupewa nafasi mwishoni mwa msimu uliopita na kocha wa sasa wa Aston Villa T.Sherwood nahofia yasije kumkuta ya kina Scot Sinclair au Jack Rodwell.

+++++++++++++++==

No comments

Powered by Blogger.