COSAFA CUP 2015 : WADHAMINI WAPATIKANA
Kuelekea katika michuano ya kombe la COSAFA 2015, Shirikisho la vyama vya soka kusini mwa Afrika COSAFA Limetangaza wadhamini wakuu wawili ambao wamepatikana kuidhamini michuano hiyo inayotarajia kuanza tarehe 17-30 mwezi Mei nchini Afrika Kusini.
Kampuni ya bia ya Afrika Kusini ambao wamekua wadhamini wakuu wa michuano hiyo kwa miaka kadhaa wameongeza udhamini wao kupitia bia ya Castle Lager lakini pia kampuni ya vinywaji ya Austria kupitia kinywaji cha Power House nao wameingia katika udhamini wa michuano ya COSAFA katika juhudi za Kampuni hiyo kujitanua zaidi kibiashara barani Afrika.
Rais wa COSAFA Seketu Patel amezishukuru kampuni hizo kwa udhamini wao na hasa kabisa akiwashukuru Castle Lager kwa kuwaamini miaka mingi mpaka kuamua kuingia tena mkataba na chama hicho.
Tanzania imealikwa kushiriki michuano ya mwaka huu ambapo timu ya taifa ya Zambia watakua wakitetea kombe waliloshinda katika michuano iliyopita mwaka 2013 wakati Angola na Comoro wao wamethibitisha kuwa hawatashiriki michuano ya mwaka huu na nafasi hizo kuchukuliwa na Ghana na Tanzania.
Michuano hiyo inasifika kuwatoa nyota kama Benjani Mwaruwari (Zimbabwe), Teko Modise na Katlego Mphela (South Africa), Chris Katongo (Zambia), Flavio (Angola), Dipsy Selolwane (Botswana), Dennis Masina (Swaziland), Essau Kanyenda( Malawi), na Tico-Tico (Mozambique)
COSAFA inaundwa na Nchi 14 ambazo ni Angola, Botswana, Comoro, Lesotho,Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, South Africa, Seychelles, Swaziland, Zambia, Zimbabwe na Congo DRC
++++++++++++++++++++++++++


No comments