MATOKEO NA WAFUNGAJI - LIGI KUU TANZANIA BARA



Jumla ya magoli manne tu yamefungwa katika mechi 3 zilizochezwa Jumamosi hii katika Ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Mabingwa watetezi Azam FC wakiwa Ugenini Manungu mambo yamezidi kuwaendea kombo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar hivyo kudhoofisha mbio zao za kuchukua ubingwa msimu huu.

Pambano kati ya Wenyeji Stand United na Ruvu Shooting limeahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Shinyanga na sasa pambano hilo litapigwa siku ya Jumatatu.

Prisons na Ndanda mambo magumu na mchezo umemalizika kwa sare tasa ya bila magoli

MATOKEO YA MECHI


● JKT Ruvu 0-2 Coastal Union
 - Rama Salim
 - Iker Obinna

● Ndanda FC 0-0 Prisons

● Mtibwa 1-1 Azam FC
 - Himid Mao Mkami
 - Mussa Hassan Mgosi

● Stand FC vs Ruvu Shooting (Imeahirishwa)

~ Edo DC

No comments

Powered by Blogger.