INSIDE UNITED : HALI YA TIMU KUELEKEA MECHI DHIDI YA MAN CITY NA TETESI ZA USAJILI
Katika INSIDE UNITED leo tutaangalia hali ya kikosi kuelekea mechi dhidi ya Manchester City itakayopigwa katika dimba la Old Trafford pia tutaangalia maswala ya Usajili na tetesi zinavyosema kutoka vyanzo mbali mbali vya habari Duniani.
Mshambuliaji Robin Van Perse ameanza mazoezi wiki hii lakini taarifa zinasema kuwa hatoweza kucheza katika mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Man City kwani hajapona vizuri na sera za kocha Louis Van gaal ni kuhakikisha mchezaji husika anapona kabisa kabla ya kumchezesha katika mchezo wa mashindano.
Mlinzi Chris Smalling yuko katika hati hati ya kucheza kutokana na kuwa majeruhi japo naye alikuwepo katika mazoezi jana wakati Mlinzi wa pembeni Luke Shaw ataendelea kuwa nje ya uwanja kutokana na maumivu ambayo hayajapona ilihali Johnny Evans yeye bado anatumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi 6 kwa kosa la kumtemea mate Papis Cisse.
KATIKA USAJILI
Taarifa nyingi duniani hivi sasa zinawahusisha wachezaji wengi kutaka kujiunga na Man united labda pengine ni kwakua United inajenga timu imra kwaajili ya miaka kadhaa ijayo.Moja kati ya habari za usajili zilizotanda ni zile zinazomuhusu Kiungo wa zamani wa united Paul Pogba ambaye inasemekana United wanawania kumsajili tena mchezaji huyu kutokea juventus na iko tayari kumpa mshahara wa paundi laki 2 kwa wiki huku kukiwa na makubaliano ya kuwauzia juventus Robin van Perse.
Pia Kiungo wa wa ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund Ilkay Gundogan anatajwa kusajiliwa na Man United mwishoni mwa msimu huu kwa ada ya uhamisho Paundi million 15 ukiwa ni makakati wa kocha Van Gaal kutaka kuimarisha kikosi licha ya kushika nafasi ya tatu hivi sasa.
Wiki iliyopita Taarifa kutoka huko huko Ujerumani zilitanabaisha kuwa Mlinzi wa Dortmund Matts hummels tayari ameshawaambia wenzake kama muda sasa umefika kujiunga na United. Huyu ni kati ya watu waliokua wanawindwa na United kwa muda mrefu nah ii itakua habari njema kwa kikosi cha United kwa kuangalia ukubwa na upana wa timu katika mashindano yote.
NOTE: TUNAKARIBISHA MAKALA TOKA KWA MPENDA SOKA YOYOTE: WASILIANA NASI KWA NAMBA 0715127272


No comments