MAN UNITED YAIMALIZA KABISA MAN CITY

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini England Manchester City wameendelea kupotea katika mbio za ubingwa baada ya kukubali kichapo cha bao 4-2 toka kwa mahasimu wao Manchester United.

Pambano hilo la watani wa jadi wa jiji la Manchester Lilipigwa katika dimba la Old Trafford nyumbani kwa Manchester United lilishuhudia mechi iliyotawaliwa na ubabe wa hapa na pale.

Man City walitangulia kupata bao kupitia kwa Sergio Kun Aguero baada ya kuunganisha pasi ya David Silva kutoka katika winga lakini United walisawazisha kupitia kwa Ashley Young.

Man United wakaongeza bao la pili kupitia kwa kiungo Marouane Fellain kisha Juan Mata akafunga goli la Tatu na badae beki Chriss Smalling akamalizia bao la nne lakini dakika za lala salama Sergio Aguero akafunga bao lake la pili kwa Man City na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 4-2.

Kwa matokeo haya Man United imefikisha pointi 65 katika nafasi ya 3 wakati Man City wamebaki na pointi zao 61 katika nafasi ya 4.

No comments

Powered by Blogger.