LIVERPOOL YATAKATA ENGLAND YAZIDI KUISOGELEA TOP 4
Liverpool imeibuka na ushindi wa bao 2-0 ikiifunga Newcastle United katika mechi ya ligi kuu nchini England katika uwanja wa Anfield.
Raheem Sterling alitangulia kuifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 8 tu ya mchezo bao lililodumu mpaka mapumziko
Kisha Joe Allen akifunga bao la pili kwa Liverpool dakika ya 70 na kumfanya kuwa mchezaji wa 15 wa Liverpool kufunga msimu huu.
Mpaka mwisho wa mchezo Liverpool wameshinda bao hizo 2-0 na kuwafanya wafikishe pointi 57 katika nafasi ya 5 ikiwa ni pointi nne nyuma ya Man City walio katika nafasi ya 4 katika msimamo.
![]() |
| Msimamo wa Ligi kuu England |


No comments