LICHA YA KUFUNGWA YANGA YATINGA 16 BORA

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Dar Es Salaam Young Africans maarufu kama Yanga wametinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika licha ya kufungwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Platinum Stars ya Zimbabwe.

Mechi hiyo ya marudiano ilipigwa katika dimba la Mandava katika mji wa Zvishavane kwa mzee Mugabe Zimbabwe.

Yanga iliingia katika mchezo wa leo ambao ulianza majira ya saa 9 za Zimbabwe sawa na saa 10 hapa nyumbani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 5-1 walioupata wiki mbili zilizopita jijini Dar Es Salaam hivyo kuwapa wenyeji mzigo mzito wa kushinda bao 4-0.

Goli pekee la Wazimbabwe hao lilipatikana dakika ya 30 ya mchezo kupitia kwa Walter Musona mpira uliogonga mwamba wa juu na kumbabatiza Barthez kipa wa Yanga na hatimaye kujaa wavuni.

Yanga walicheza kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kutoruhusu bao lolote zaidi ya hilo moja na kufanya mchezo huo kumalizika kwa kipigo cha bao 1-0 ambacho Yanga wamekipata lakini wanasonga na kutinga hatua inayofata ya 16 bora.

_________________________

Kikosi cha Yanga SC leo;
__________________________

Ally Mustafa ‘Barthez’,
Juma Abdul,
Oscar Joshua,
Mbuyu Twite,
Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’,
Said Juma/Kevin Yondan aliingia dakika ya 46,
Simon Msuva/Danny Mrwanda aliyeingia dakika ya 88,
Haruna Niyonzima,
Amisi Tambwe,
Mrisho Ngassa
Salum Telela.

*********************************

No comments

Powered by Blogger.