ARSENAL HII HATARI YAIKANDAMIZA LIVERPOOL 4

Arsenal imepanda mpaka nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu Nchini England baada ya kuwakandamiza bila Huruma Liverpool bao 4-1.

Arsenal ambao wameonekana kuimarika hivi sasa hasa baada ya wachezaji waliokua majeruhi kupona licha ya kupata ushindi huo mkubwa lakini pia walitandaza soka la uhakika lililowafanya Liverpool kupoteana kabisa mchezoni.

Arsenal walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Hector Belarin dakika ya 37 kabla ya Mesut Ozil hajafunga la pili dakika tatu badae na Alexis Sanchez kumalizia la Tatu dakika moja kabla ya kwenda mapumziko na kufanya mechi hiyo kwenda mapumziko Arsenal wakiwa mbele kwa bao 3-0.

Kipindi cha Pili Arsenal walipunguza kasi wakicheza pasi nyingi na kuvutia watazamaji huku Liverpool wao wakiwa wanahaha kutaka kurudisha magoli hayo na hata kusababisha Amre Can kulimwa Kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.

Nahodha wa Liverpool Jordan Handerson aliifungia timu yake bao pekee kwa njia ya penati kabla ya Olivier Giroud hajapiga bao la 4 na kumaliza mchezo huo kwa Arsenal kuibuka na ushindi mnono wa Bao 4-1 Liverpool akiathiriwa na magoli hayo.

+++++++++++++++++++++*

No comments

Powered by Blogger.