IMETHIBITISHWA MECHI YA YANGA LIVE KATIKA AZAM TV
Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinasema kuwa Azam media kupitia kituo chake cha Azam Two wataonyesha moja kwa moja matangazo ya soka kati ya wenyeji Platinum FC ya Zimbabwe dhidi ya Yanga ya Tanzania kuanzia saa 10 jioni saa za hapa Tanzania.
Pia Azam One itarusha pambano la kombe la Shirikisho Afrika kati ya URA ya Uganda na Orlando Pirates ya Afrika Kusini muda huo huo wa saa 10 alasiri.
Mechi kati ya Kagera Sugar na Simba itarushwa kupitia chanel namba 100 kuanzia saa 10 na nusu ambayo mara nyingi huwa ni chanel ya Matangazo kwa wenye king'amuzi cha Azam Tv.

Well
ReplyDelete