KIMEO : MALKY MACKAY ATIMULIWA WIGAN



Imekua ni mkosi juu ya mkosi kwa kocha aliyeipandisha Cardiff City ya England Malky Mackay ametimuliwa na mwajiri wake klabu ya Wigan inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England (Championship)

Ikumbukwe Mackay alipata kazi ya kuifundisha Wigan mwezi Novemba mwaka jana baada ya kukaa muda mrefu bila timu alipotimuliwa Cardiff City.

Wigan imepata pointi 19 tu katika michezo 24 iliyocheza chini ya kocha huyo ikiwa haijawahi kushinda mechi yoyote katika dimba lake la nyumbani la DW na kufanikiwa kupata pointi tatu tu akiwa na Wigan nyumbani.

Wigan leo wameambulia kichapo cha bao 2-0 toka kwa Derby County na kupoteza kabisa matumaini ya kubaki katika Ligi daraja la kwanza inakamata nafasi ya 23 katika msimamo ikiwa na pointi 35 huku ikiwa imebaki michezo mitano.

×××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.