SIMBA YATAKATA SHINYANGA YAWAKALISHA KAGERA.



Na: Bab Chicharito, Shinyanga

Pambano la Ligi kuu Soka Tanzania Bara kati ya Simba ya Dar Es Salaam na Kagera Sugar lililopigwa katika dimba la Kambarage Mjini hapa limemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-1

Mchezo huo ambao ulipaswa kuchezwa Juzi Jumamosi uliahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini hapa na ndipo Bofi ya ligi wakishauriana na vilabu vyote viwili walikubaliana mechi hiyo kuchezwa Leo na pambano hilo kupigwa kuanzia majira ya saa 9 alasiri.

Simba walionekana kuapania vilivyo mchezo huo na mpaka kipindi cha kwanza kinaisha walishapata nafasi 5 za kufunga lakini bahati haikua yao na kufanya mchezo huo kwenda Mapumziko zikiwa Sare ya bila kufungana.

Ibrahim Ajib,Danny Sserunkuma,Ramadhani Singano na Emmanuel Okwi walikua na kazi kubwa kuhakikisha hawafanyi makosa waliyofanya kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao la kwanza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Ajib kumaliziwa na Singano na kuandika bao la kwanza.

Kagera Sugar walisawazisha dakika chache badae kupitia kwa Mkali wa Mabao Rashid Mandawa na kumwacha Kipa Manyika Peter akishindwa la Kufanya.

Simba walifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Kagera na moja ya shambulio hilo lilizaa penati ambayo mabeki wa Kagera walikua wakihangaika kuuokoa mpira na ndipo ulipomgonga beki mmoja wa Kagera katika mkono na ndipo mwamuzi akaamua ipigwe penati ambayo Ibrahim Ajib hakufanya ajizi akafunga na kuihahikishia Simba pointi tatu muhimu.

KIKOSI CHA SIMBA LEO

Manyika Peter
Masoud Chollo
Tshabalala
Isihaka Rashid
George Owino
Awadh Juma
Said Ndemla
Ramadhani Singano
Emmanuel Okwi
Ajib\ Twaha
Dany Sserunkuma/Idrisa Rashid (baba ubaya)

No comments

Powered by Blogger.