UBINGWA WAZIDI KUIKIMBIA MAN CITY.



Ndoto za Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City zimezidi kufifia baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Crystal Palace.

Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Selhust Park jijini London lilishuhudia Palace wakipata goli la kwanza dakika ya 34 kupitia kwa Gleen Murray na mpaka mapumziko Palace walikua wakiongoza kwa goli hilo moja.

Kipindi cha pili kilitawaliwa na Ufundi mwingi huku kila timu ikijitaidi kuondoka na pointi Zote lakini ilikua Palace ndiyo waliofunga tena kupitia kwa. Jason Puncheon dakika 3 tu tangua kuanza kwa kipindi cha pili.

City walijikwamua na kupata bao pekee katika mchezo huo kupitia kwa Yaya Toure goli ambalo halikubadilisha matokeo ambayo yamewaacha Man City katika nafasi ya 4 na mechi ijayo itakua dhidi ya Wapinzani wao Man United katika uwanja wa Old Trafford.

No comments

Powered by Blogger.