YANGA NA JKT RUVU HAPATOSHI TAIFA LEO
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa na vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Dar es Salaam Young Africa maarufu kama Yanga wanajituma uwanja wa Taifa leo kucheza na JKT Ruvu.
Katika pambano hilo la 19 kwa Yanga na la 20 kwa JKT Ruvu litapigwa jioni hii jijini Dar huku Yanga wakiwa wanaongoza Ligi hiyo wakiwa na pointi 37 wakiwa wameshacheza michezo 18 wameshinda 11, wakitoka sare mara 4 na kufungwa mara 3.
JKT Ruvu wao wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na 24 wakiwa tayari wameshacheza michezo 19 wakishinda 6,kutoka sare 6 na kufungwa mara 7wanakamata nafasi ya 5.
Wachezaji wote walioitwa katika timu ya Taifa ya Tanzania kutoka Yanga wamebaki kwaajili ya pambano hilo ambalo Yanga wanahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza ligi.
++++++++++++++++++++++

No comments