●●INSIDE UNITED ●● HAWA NDIYO WACHEZAJI WANAOWINDWA NA MAN UNITED HIVI SASA.
![]() |
| Felipe Anderson kushoto |
Wikiend iliyopita wakati Man United ikisherekea ushindi ugenini dhidi ya Liverpool wasaka vipaji wetu wao walikua bize kufatilia nyendo za nyota watatu ambao kocha Louis Van Gaal amependekeza wasajiliwe.
Msaka vipaji Jim Lawlor yeye ilibidi asafiri mpaka Italia kuangalia mechi kati ya Lazio na Verona mechi iliyopigwa siku ya Jumapili lengo kuu likiwa ni kuwaangalia wachezaji wawili Kiungo Mbrazil Felipe Anderson na Beki wa Kati Raia wa Uholanzi Stefan de Vrij wanaokipiga katika klabu ya Lazio ya Italia.
![]() |
| Stefan de Vrij |
Felipe Anderson ambaye ni rafiki mkubwa wa Neymar wa Bacelona ni bonge moja la kiungo ambaye Lazio wamempa mkataba mpya unaoisha mwaka 2020 ameshafunga magoli 10 msimu huu anawindwa pia na Man City,Arsenal na Liverpool.
Kwa Upande wake msaka vipaji mwingine Mspaniola Carlos Ruiz alikua uwanjani siku ya Ijumaa katika mechi kati ya Valencia na Elche lengo kuu likiwa ni kumwangalia beki wa Valencia Nicolas Otamend mwenye miaka 27 ambaye katika mkataba wake ili umtoe pale Valencia inabidi kutoa paundi milion 37.
![]() |
| Otamendi |
Kwa leo ni hayo tu kutoka katika INSIDE UNITED tukutane kesho kwa habari zaidi zinazoihusu Man United.
Usiku mwema.



No comments