SABABU 10 KWANINI TIMU ZA ENGLAND ZIMESHINDWA KUFANYA VIZURI KWENYE MICHUANO YA ULAYA MIAKA YA HIVI KARIBUNI.
1: The third Newton's law of Motion.Newton aliwahi kusema kwamba "For every action there is an equal and opposite reaction" kanuni hii ndo inayozikumba timu za England kwa sasa.Wakati dunia ikishuhudia miaka ya 2000-2008 timu za ujerumani zikishindwa kufanya vzuri kwenye michuano ya ulaya na ikafikia kipindi wakawa wanashindwa kupitisha hata timu moja Robo fainali.Kwenye Nyumba za starehe nchini England zilikuwa zinajaza Waingereza wakifurahia Timu zao zikiwa tatu kwenye hatua ya nusu fainali.Wakasahau kuna Maisha baada ya mafanikio ni jinsi gani utaweza kuishi kwenye mafanikio yako kwa muda mrefu.Tulichoshuhudia baada ya hapo ni baba aliyekuwa anamiliki gari kumrithisha mtoto wake Vyuma chakafu.Wakati baba wa Jirani akichukua vyuma chakafu na kutengeneza gari kwa ajili ya urithi wa mtoto wake.
2:Kizazi cha dhahabu cha Wajerumani na Wahispania.Kuanzia 2009 Bayern munich imefika mara nne nusu fainali na kufanikiwa kuingia fainali tatu na wakashinda moja 2013.
Barcelona wamefika mara nne nusu fainali kwenye michuano 6 iliyopita na wakashinda mbili 2009 na 2011.
Sitaki kuiongelea R.Madrid iliyofika nusu fainali 3 na kuchukuwa moja ila A.Madrid na Borrusia Dortmund ni moja ya vizihilisho vya vizazi hivi vya dhahabu kwenye nchi hizi mbili.Vizazi hivi zimekuwa mwiba mchungu kwa timu za England.Mfano misimu mitano iliyopita kuanzia 2009 ni Chelsea pekee iliyofanikiwa kuitoa timu kutoka Hispania na Ujerumani .Ilifanya hvo 2012 ilipoitoa Barcelona na ikafanya hvo kwa bayern mwaka huo huo kwenye fainali ya UEFA.Kwenye michuano mitano iliyopita Ujerumani imetoa 40% ya wanafainali.Wakati hispania ikitoa 30% na England ikitoa 20%.
3:Sera ya wachezaji wa nyumbani.Kuanzia miaka ya 2000 kiwanda cha kufyatua wachezaji kilianzishwa nchini Ujerumani.Kiwanda hiki kilifyatua matofali bora na imara ambayo yalitumika kujenga nyumba bora kwa mzee Bayern Munich na kwa kijana Borrusia dortmund.Kiwanda hiki kilimwezesha kijana Borrusia dortmund kuwa na wachezaji 10 waliohusika kumfunga Manchester City 2012.Kuna faida sana ya kuwa na wachezaji wa nyumbani kwenye kikosi kwa sababu huwa tayari wamelishwa damu ya uzalendo wa kuipigania nchi yao achana na wale waliokuja kuchukua hela na kupigania kutokuwa majeruhi kuliko kupigania timu.
4:Kipindi cha Majira ya Baridi.Wakati shakira akimchua misuli Gerrarld Pique na kumhimiza aende ufukweni kufanya mazoezi mepesi Vincet kompany yeye anahangaika kumkaba Diego Costa na kuishia kupata majeruhi yanayomweka nje kwa muda mrefu na akirudi inamchukua muda mrefu kurudi kwenye kiwango chake na Anakutana na Messi ambaye alitumia Muda wa majira ya baridi kupumzisha misuli yake.Kwwnye siku 41 ambazo Bayern munich amepumzika tokea December 19 Man city kacheza michezo 8 ya ushindani .Timu inacheza Boxing day..Mwaka mpya ina mechi Afu Weekend ina FA CUP na ni kipindi cha baridi.
5:Kupoteza Kuta Imara za ulinzi za Timu za England.Man U walihitaji uimara wa Vidic na Ferdinald kupata clean sheet kwao mbele ya Barcelona iliyowasaidia kuwatoa.Sitaki kuzungumzia ukuta wa Sol Campell na Kolo Toure au ubora wa Sam hypia na Jamie Carragher ila nazungumzia ubovu wa ukuta Wa Martin na Vincent pale Man city au ukuta wa pale Arsenal usiojua kukaba mashambulizi ya kushtukiza kwenye kuzazi hiki cha kina Robben na Messi.
6:Pressure ya Ligi kuu ya England .Ushindani wa EPL hvi karibuni umesababisha Timu zinazofuzu michuano ya ulaya inashindwa kucontrol pressure hiyo mpaka kwenye michuano ya Ulaya.Unakutana na Bayern inayoongoza kwa utofauti wa point nyingi na imetoka kucheza Ijumaa na kushinda bila pressure kwa 7-0 afu wewe Burnely kakulazimisha draw na umeweka kombe lako rehani
7:Kushindwa kuajiri mpira wakati wa mechi.Hakuna silaha kubwa kwa timu kama kuwa mwajiri wa mpira wakati wa mechi .Hii hufanya Timu kuushurutisha mpira ipendavyo.Kwa miaka ya hv karibuni hiki kitu kimekosekana Kwa timu za England .Ngoja nikupe mfano Wakati Barcelona anaongoza goli 1 pale Nou camp dhid ya Manchester city.Messi aligusa mpira mara 116 kuzidi Timu ya Man City kiujumla.Unapokuwa na mpira ni silaha tosha ya kuzuia na kushambulia.
8:Kupungua kwa "Winning Mentality "za timu za England.Ngoja nikupe mfano.Kwenye mechi zote walizokutana na Bayern munich hivi karibuni Arsenal wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani hawakuwa na hali ya ushindi walicheza kwa kuzuia muda mrefu hiki kitu hakikuwepo kwa Arsenal ya miaka mitano iliyopita iliyokuwa na njaa ya ushindi kila mechi.
9:Kutotumia vzuri viwanja vya nyumbani.Ukiangalia vzuri msimu huu Timu zote za England zimetolewa kwa sababu ya Kutotumia vzuri viwanja vyao.Achana na utoto wa Arsenal pale Emirates dhid ya Monaco au ubovu wa city wa kipindi cha kwanza pale Etihad ila kichefufu zaid ni pale Mtaalamu wa michezo hii ya mitoano Jose alivyoshindwa kuonesha utaalamu wake mbele ya PSG pale darajani
10: Kutokuwa na Bahati .Hii inaweza ikawa siyo sababu ya msingi kwa haraka haraka.Ila kiukweli ilihitajikia bahati 1999 kwa united kufanya maajabu makubwa ya kutoka nyuma na kusawazisha inawezekana mwaka huo hukuangalia vipi pale Instanbul.Hakika liverpool ikiwahitaji bahati kutoka nyuma ya magoli 3 na kuchukua ndoo.Unaweza ukasingizia mwaka huo 2005 hukuwa mshabiki na mfuatiaji mzuri vipi ya mwaka 2012 ? Chelsea kuchukua mbele ya kikosi bora cha Bayern Munich hakika bila kupepesa bahati ndo iliyowabeba hasa hasa nikikumbuka seke seke la Robben.Hizi bahati haizitembelei timu za England kwa siku za hivi karibuni.Hata ukiwa na kikosi bora unahitaji bahati.Kamuulize Sir Alex.Ukiona huipendi Man Utd Nenda Anfield wakupe majina mawili ya makocha wenye mafanikio makubwa ndani ya klabu na ligi kuu ya England Afu wafuate kawaulize kuhusiana na bahati kwenye mpira.
Sikutaka kuzungumzia Vyombo vya habari vya England kumkuza Wilshere mbele ya Iniesta. Na kusababisha wachezaji wa England kuwa ghali na kubweteka zaidi.
Ila jiulize Man city anacheza na Man U jumapili afu Jumanne anakutana na Bayern aliyecheza Ijumaa .Unategemea kipi kitatokea ?



No comments