DE GEA AMPONZA SKRTEL WA LIVERPOOL AFUNGIWA MECHI TATU


Beki wa Liverpool Martin Skrtel amefungiwa kutocheza mechi 3 zinazokuhusu cha,a cha soka nchini England baada ya kupatikana na kosa la kumkanyaga kwa makusudi kipa wa Manchester United David de Gea.

Baada ya kupewa muda wa kujitetea kwanini asipewe adhabu na utetezi wake kutojitosheleza imeonekana beki huyo ana makosa na sasa atatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 3 na hii ni baada ya kupitia picha za video ambazo zinamwonyesha akimkanyaga kwa makusudi David De Gea katika dakika za mwisho za mchezo uliomalizika kwa ushindi wa 2-1 ambao Man United waliupata.

Beki huyo nyota raia wa Slovakia mwenye miaka 30 alifanya kosa hilo katika mchezo huo lakini mwamuzi Martin Atkinson hakuona tukio hilo.

Michezo ambayo Krtel ataikosa ni mchezo wa ugenini dhidi ya Arsenal, ule wa nyumbani dhidi ya Newcastle na ule wa marudiano dhidi ya Blackburn katika kombe la FA hatua ya Robo fainali.

Katika mchezo huo Steven Gerard nae alipata kadi nyekundu baada ya kufanya kosa km la Skrtel na mwamuzi kuliona.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.