SIMBA YAFANYA KWELI TAIFA YAIFUMUA RUVU BILA HURUMA.
Baada ya kichapo walichokipata katikati ya wiki dhidi ya Mgambo JKT pale Mkwakwani timu ya Simba leo imerekebisha makosa na kuibamiza Ruvu Shootinga mabao 3-0 katika pambano safi na la kuvutia lililopigwa katika dimba la Taifa
Iliwabidi Simba kusubiri mpaka kipindi cha pili ili kupata ushindi huo kwani mpaka mapumziko Timu hizo zilitoshana nguvu na kumaliza dakika 45 zikiwa bila bila.
Simba itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa magoli lukuki kikpindi cha kwanza kwa washambuliaji Emmanuel Okwi na Ibrahim Ajib kushindwa kufunga katika nafasi za wazi kabisa.
Magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib kwa penati dakika ya 60 baada ya beki wa Ruvu kumfanyia madhambi Awadhi Juma. Dakika moja baadae Awadh Juma alifunga bao la pili na Elias Maguli akamalizia bao la 3 dakika ya 75.
Simba imefikisha pointi 32 baada ya kucheza michezo 20 ikikamata nafasi ya 3.
++++++++++++++++++++++

No comments