KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : LIVERPOOL VS MAN UTD, WALICHOSEMA WAPENDA SOKA




Karibuni katika KIJIWE CHA WAPENDA SOKA leo ambapo kijiweni leo mvua imezingua kwahiyo watu hawajapata muda wa kutosha kujadili kuhusu mechi hii ila tumeweza kupata maoni ya Wapenda Soka wachache ambao wamefunguka kama wanavyojua na nini maoni yao kuhusu pambano hili.

EDO DANIEL CHIBO


- Hii ndiyo mechi kubwa zaidi katika historia ya ligi kuu Nchini England. Tofauti na Dabi ya Manchester hii huvuta hisia za mashabiki wote wa Soka ambao wanafatilia soka la England.

Zinakutana timu mbili ambazo mafanikio yao yanakimbizana Man Utd ikiwa imepata mafanikio makubwa kipindi ambacho Liverpool ilikua dormant (Imelala)

Liverpool ikiwa imeshanyakua ubingwa wa ligi kuu England Mara 18 Man United imenyakua mara 20 lakini ndani ya miaka 20 iliyopita Man United ndiyo imetawala zaidi.

Mara ya mwisho Liverpool kuchukua ubingwa wa 18 wa England United ilikua imeshachukua ubingwa huo mara 7 tu na Tangu mwaka 1992 United imeweza kuchukua ubingwa mara 13 huku Liverpool wakibaki pale pale.

- Upinzani baina ya timu hizo ulianzia kisiasa zaidi na kuhamia katika mpira kwani miaka zaidi ya 100 iliyopita Bandari ya liverpool ilikua ndiyo inatumika kusafirishia mizigo toka katika jiji la Manchester ambalo lilikua lina viwanda vingi  na hali ikaonekana meya wa jiji la Liverpool alikua akiibania mizgo toka na kwenda Manchester

Lakini baadae Manchester Ikajenga bandari yake na hapo uhasama ukabaki katika soka baina ya vilabu hivyo viwili Manchester United ikilibeba jiji la Manchester na Liverpool ikilibeba jiji la Liverpool ambalo liko kusini mwa England.

Huu ni mchezo wa pili msimu huu kwa timu hizo mechi ya kwanza ikiisha kwa United kuibuka na ushidi wa bao 3-0 katika dimba la Old Trafford mechi ambayo iliizindua Liverpool ambayo ilikua na mwendo wa kusuasua katika ligi na tangu kipindi hicho imeweza kushinda mechi zake zote za ligi na kurudi katika nafasi ya kugombania nafasi nne za juu katika msimamo.

- Tofauti na mapambano ya miaka iliyopita pambano la mwaka huu ni la kugombea zaidi nafasi ya kucheza katika ligi ya mabingwa barani Ulaya mwakani.

Wakati United ikiwa katika nafasi ya 4 na Liverpool nafasi ya 5 tofauti ya pointi kati ya wawili hao ni pointi mbili tu. Mchezo wa leo kama ilivyokuwa kwa michezo mingine baina ya timu hizo hutawaliwa na ubabe wa hapa na pale na mara nyingi kadi hutawala.

Tunaenda kushuhudia mchezo mzuri huku United ambayo miaka mingi imekua ikitawala kwa soka la kutegemea winga msimu huu wamekuja na soka la kumiliki mipira zaidi na kutumia mipira mirefu kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji huku Liverpool chini ya Brendan Rodgers ikitumia pasi fupi fupi na mpira wa kasi kuelekea katika lango la wapinzani.

Uwepo wa Fellain katika kikosi cha United itakua njia tosha ya kuharibu mashambulizi ya liverpool japokua nauona pia kama unaweza kuihatarisha Man United kwani Fellain mara nyingine huwa na hasira zisizo na maana.

Liverpool wao wana watu watatu wenye kasi na akili sana ya kutengeneza Masambulizi Raheem Sterling,Daniel Sturadge na Coutinho hawa ni watu hatari sana kama viungo na mabeki wa United watawaruhusu kuingia katika 18.

Kwa maoni yangu Man United Itashinda katika mchezo huo bao 2-1 au 3-1

+++++++++++++++++


ZAHIR BILAL


Kuelekea mechi ya Liverpool vs Manchester United Ningependa tuangalie mambo muhimu yanayoweza kuamua mechi hiyo itakayopigwa kwenye dimba la Anfield

1. MBINU 

Makocha wote wawili ni wataalamu hasa linapokuja suala la mbinu na namna ya kukabiliana na mpinzani,nategemea Liverpool kuingia na mfumo wa 3-4-3 ambao umezaa matunda kwa kiasi kikubwa tangu wameanza kuutumia with high pressing game, quick counter attacks, style yao ya pasi fupi fupi na aina ya wachezaji walionao lazima wataisababshia matatizo United pale nyuma hasa yule Mbrazil Coutinho ambaye yupo kwenye kiwango kizuri mno ukijumlisha na uwezo wa Sterling  beki ya United inatakiwa iwe vizuri

kwa upande wa United LVG anaweza kubaki na kikosi kile kile cha juma lililopita au akafanya mabadliko machache lakini pia anaweza akabadili kabisa mfumo  kutokana na mechi ya leo ilivyo inaweza kuwa  4-3-3 au 4-4-2 flat kama Valencia atacheza winga baada ya kupona kwa Rafael au 3-5-2 hii iko 50-50 kutokana na ukosefu wa beki wa kati anayetumia mguu wa kushoto japo Blind anaweza kucheza hiyo nafasi lakini sio kwa ufasaha

United leo watawavizia zaidi Liverpool japo LVG anapenda timu yake ikae na mpira..ikiwa Liverpool wakiingia na 3-4-3 watakua wamejiweka wazi nyuma na hapa United itamuhitaji Ange Di Maria aliyemlambisha sakafu Puyol zile zig zag zake za msimu uliopita zitahitjika zaidi hapa

2: TAKWIMU 

Takwimu za United ugenini msimu huu si nzuri wameshinda mechi nne tu na wanaenda Anfield kati ya viwanja vigumu pale uingereza wakiwa hawana rekodi nzuri pia katka mechi 5 zilizopita baina ya timu hizo wameshinda 1 kwa magoli ya RvP na Rafael  msimu wa 2012/13

3: WAYNE ROONEY

Nahodha wa United Wayne Rooney mara nyingi hupotea mchezoni katika mechi na Liverpool lakini kwa sasa ndio kiongozi pale United atatakiwa awe mfano leo kama United wakitaka ushindi wanamuhitaji huyu jamaa awe katika kiwango chake

4: HENDERSON/GERARD vs CARICK/HERRERA


Hawa ni watu ambao wananifanya niliangalie pambano hili kwa jicho la tatu kwani atakayemfanya mwenzie akimbize kivuli chake kwenye kiungo itatoa mwanya kwa timu yake kushinda.

Liverpool wao wana mzoefu (Steve Gerard ) wanajumlisha  na kazi nzuri anayoifanya Henderson wakati  United wana Mr Compuser (Michael Carick ) na faida pia kuwa na  Dynamism (Herrera)

5: FELLAIN NA COUTINHO 

Hawa ni watu ambao wanaweza kuamua matokeo ya mechi hii fungua macho yako kuangalia pasi za hatari za Philipo Coutinho au mipira ya juu inavyofanyiwa ustaarabu na Big Fella.

Utabiri:Shilingi  yangu bado imesimama ila naona droo ya 1:1

.... Kutoka KIJIWENI ni hayo tu tuliyoweza kukuandalia katika mechi hiyo ambayo itaanza majira ya saa 10 na nusu jioni.

Asanteni.


1 comment:

  1. Uchambuzi mzuri, mimi natabiri sare ya goli zaidi ya moja. GGMU!

    ReplyDelete

Powered by Blogger.