●● INSIDE UNITED ●● MAN UNITED YAZIDI KUPAGAWISHA YAIBAMIZA LIVERPOOL KWAO.

Red card : Steve G
Katika INSIDE UNITED leo tunaangalia ushindi wa bao 2-1 ugenini dhidi ya Liverpool
++++++++++++

Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi kwa kuibamiza Liverpool bao 2-1 katika pambano la Ligi kuu nchini England katika dimba la Anfield.

Man United ambayo imeonekana kuwa na mechi ngumu tangu kuanza mwezi wa 3 imezidi kudhihirisha kuwa timu inazidi kuimarika na kupata Ushindi huo ugenini katika uwanja ambao mara nyingi umekua ukiwasumbua.

Alikua Juan Mata aliyefunga magoli yote mawili ya Man United akifunga goli la kwanza baada ya kupokea pasi ya Ander Herrera kipindi cha kwanza huku lile la Pili akifunga kwa Tik tack baada ya kutengenezewa vyema na Angel Di Maria ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ashley Young.

Jambo la kukumbukwa katika mchezo huo ni kwa Steven Gerrard aliyeingia kipindi cha pili wakati kinaanza akichukua nafasi ya Adam Lallana kucheza kwa sekunde 45 tu baada ya kutolewa nje na mwamuzi Martin Artinkson kwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga kwa makusudi Ander Herrera.

Jambo lingine la kukumbukwa ni nahodha wa United Wayne Rooney kukosa penati baada ya mwamuzi kuipa Man United penati kufatia kufanyiwa madhambi Daley Blind na penati hiyo kudakwa kiufundi na Simon Mignolet.

Goli la Liverpool lilifungwa na Daniel Sturadge na kufanya matokeo mpaka mwisho kuwa 2-1 Man United wakiibuka na ushindi.

Kwa matokeo hayo Man United inasogea kwa pointi mpaka pointi 59 katika nafsi ya 4 ikiwa ni pointi moja mbele ya Arsenal wanaokamata nafasi ya 3 na pointi mbili nyuma ya Man City.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.