KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : HAYA NDIYO MAWAZO YA WAPENDA SOKA KUHUSU ELCLASICO
Baada ya kushuhudia pambano kali pale Katika dimba la Anfield na United kuibuka na ushindi wa bao 2-1 sasa tunaelekeza mawazo yetu katika El Clasico na machache kati ya mengi tuliyoyaongea haya ndo tuliyofanikiwa kukuletea
MANATSON SALEWA
Kwa maoni yangu mimi Barcelona yuko nyumban hii inamuongezea ari na nguvu ya kufanya vizuri sana sana katika pambano la leo na katika siku za hivi karibuni Barcelona amekua akifanya vizuri katika mechi kama hizi zinazopigwa Nou Camp.
Kuwepo nyumban sio kitu pekee kinachoipa nguvu Barcelona lakini kwa siku za hivi karibuni Barcelona imeimarika sana na hii ni baada ya kuchapwa na Malaga akiwa nyumban na kwa hali ilivyo hii mechi ina mtazamo wa kipekee kwa wachezaj kocha na mashabiki
MESSI SUAREZ NEYMAR
Hawa watu hivi sasa muunganiko wao unazidi kupendeza na inaonekana kabisa sasa kwa kasi yao na pasi za haraka haraka huku wakizalisha magoli mengi katika siku za hivi karibuni zaidi ya 95% japo Neymar bado ana utoto ila kwa hii mechi nadhani ataingia kivingine na Ana record nzuri kwenye El ClassicoTuje kwenye kiungo cha Barcelona. Hawa jamaa kiungo chao kimekaa vizuri sana ukizingatia hakuna majeruhi wa kutegemewa katka eneo hili ukimwangalia mtu kama Ivan Rakitic huyu jamaa Ana uwezo wa kipiga pasi na pia kufunga na kutengeneza magoli hvyo Madrid itawabidi wawe makini sana.
Nikitupia jicho Real Madrid hawa jamaa hawakuanza ligi kwa kasi ila waliimarika kadri ligi iliposonga mbele na hadi wakaongoza ligi kabla ya kushushwa na Barcelona wiki iliyopita.
Tukianza kwa kipa Iker Cassilas amepungua sana makali yake huyu si yule Cassilas tuliemzoea kwani anafungwa magoli ya kizembe hasa mipira iliyokufa na anashindwa kupanga mabeki vizuri.
Ukija kwenye nafasi ya ulinzi hapa kuna tatizo kwani Real Madrid asharuhusu magoli mengi sana ukilinganisha na mpinzani wake mabeki wake wanawaza kushambulia zaidi kuliko kulinda na hivyo kuathiriwa na mashambulizi ya ghafla.
Kiungo cha Real Madrid kinakosa ubora wake ila uwepo wa Luka Modric ambaye ndiyo muuaji mkuu wa timu wapinzani na msshambulizi ya Madrid huanzia katika miguu yake.
Huyu Tofauti na Toni Kroos yeye anajua kukaba na yuko makini sana tofauti na Kroos ambaye kama ataanza basi itampasa kuwa makini sana
Eneo la ushambuliaji sina shaka nalo kabisa japo hivi karubuni kuna tetesi za chini chini kua Cristiano Ronaldo na Gareth Bale haziivi ila mimi nadhani mpira kazi hawa jamaa lazima wafanye kazi kwa pamoja kumuua ADUI Leo.
Mechi kama hizi mara nyingi muuaji mkuu ni Karim Benzema na kama huyu jamaa akiwa katika ubora wake basi ni dhahiri magoli yatapatikana.
Ubashiri wangu Barcelona anashinda 2-1
#++++++++++++
EDO DANIEL CHIBO
Mechi ya wapinzani wa jadi katika soka nchini Spain yani mvuto wa mechi hii unaikamata dunia yote. Wapenda Soka wengi watakua katika Luninga zao usiku wa leo
Kwa upande wangu najaribu kuangalia historia ya hizi mechi na pengine toka hapo nitakuja na utabiri wangu
Real Madrid wameshinda Mechi mbili zilizopita katika El Clasico na kama watashinda leo basi watafikiaha mechi tatu mfululizo wanaibuka na ushindi na hii itakua mara ya kwanza tangu mwaka 1978.
Lakini tusijisahau pia Real Madrid ni ngumu sana kupata ushindi Nou Camp kwani Barcelona haijawahi kufungwa na Real Madrid nyumbani wakati kama huu wanaongoza Ligi mara ya mwisho kupoteza wakiwa wanaongoza ligi ilikua msimu wa 1929/1930.
Kwa mwaka 2015 pekee Lionel Messi amefunga magoli 17 katika La Liga hii ni zaidi ya wakali wa mabao wa Real Madrid kwa pamoja yani magoli ya Benzema,Bale na Ronaldo hayafikii haya ya Messi kwa mwaka huu 2015 kila mmoja kafunga goli 5.
"The form book goes out of the window for the Clasico," Barca defender Gerard Pique said.
Licha ya Barcelona kushinda katika mechi 9 kati ya 10 ilizocheza lakini pambano la El Clasico hubaki kuwa nusu kwa nusu yani yoyote anaweza kushinda hapa inapaswa tu wale wakali wawe katika viwango bora.
Real Madrid wanaweza kupoteza kama wataendekeza ubinafsi kila mshambuliaji kutaka kuonyesha anajua wakati Barca wao hilo sio tatizo kwao kwani Messi,Suarez na Neymar wamekua wakisaidiana kupata ushindi kwa ajili ya timu.
Tunahitaji kumwona Cristiano Ronaldo na Messi wakiwa katika ubora wao ili kunogesha pambano hili.
Utabiri wangu ni sare ya bao 2-2
Asanteni sana.

No comments