LUIS SUAREZ AWALIZA REAL MADRID


Luis Suarez amefunga goli lake la kwanza katika El Clasico akiiongoza timu yake ya Barcelona kushinda nyumbani kwa mbao 2-1 wakiwafunga wapinzani wao wakubwa katika soka la Spain klabu ya Real Madrid.

Iliwachukua dakika 19 tu Barcelona kufunga bao la kwanza kupitia kwa beki wake Mathieu kabla ya Criatiano Ronaldo hajasawazisha na kuifanya mechi hiyo kwenda Mapumziko magoli yakiwa 1-1

Kipindi cha pili Barcelona waliongeza bao kupitia kwa mshambuliaji wake Luis Suarez bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuwafanya Barcelona kuzidi kupaa katika uongozi wa Ligi ikiwa na tofauti ya pointi 4 dhidi ya Real Madrid inayoshika nafasi ya 2.

++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.