REAL MADRID HALI MBAYA YAKUBALI KICHAPO TOKA KWA BILBAO
Real Madrid wameendelea kupoteza matumaini ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu nchini Spain baada ya kulambishwa bao 1-0 toka kwa Athletic Bilbao.
Mchezo huo wa La Liga ulipigwa katika dimba la San Mames Barria nyumbani kwa Athletico Bilbao ulimalizika kwa kipigo kingine na kuwapa mwanya Barcelona kuwapumulia kwa karibu.
Bilbao walipata bao pekee katika mchezo huo dakika ya 20 kupitia kwa Aritz Aduriz goli ambalo lilidumu mpaka mwisho
Kwa matokeo hayoReal Madrid wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 61 huku wakiwa wameshacheza michezo 26 huku Barcelona wakiwafatia wakiwa na pointi 59 huku wakicheza michezo 25.
Bilbao wao wamesogea mpaka nafasi ya 8 wakiwa na pointi 33 baada ya michezo 26.
No comments