AZAM YATAKATA LIGI KUU YAIOMBEA YANGA IPOTEZE KESHO.



Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi na klabu ya Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara Didier Kavumbagu leo alifunga bao muhimu na bao la pekee wakati Azam wakiibamiza JKT Ruvu kwa bao 1-0.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex Azam walipata goli hilo kupitia kwa Kavumbagu aliyeunganisha mpira wa Shomary Kapombe

Matokeo yanawapandisha Azam ambapo sasa wamefikisha pointi 30 moja nyuma Yanga wanaoongoza.

MATOKEO MENGINE

Coastal Union 2-2 Kagera Sugar

No comments

Powered by Blogger.