HARRY KANE AZIDI KUWA MTAMU 



Mshambuliaji wa England na klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane amezidi kuonyesha umwamba wake kwa kufunga mabao mawili yote katika mechi ya Ligi kuu ya England dhidi ya Queens Park Rangers.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa ushindi wa bao 2-1 ambao Tottenham waliupata mabao yote mawili yalifungwa na Harry Kane akifunga bao la kwanza katika dakika ya 34 akiunganisha pasi murua ya Andros Townsend na lile la pili alilifunga dakika ya 69.

QPR ambao balaa la kushuka daraja limewakomalia walijitahidi na kupata bao la matumaini dakika 76 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo hao ya 2-1.

Tottenham kwa matokeo hayo wameongeza ushindani katika msimamo wa Ligi kwani wameweza kufikisha pointi 50 pointi moja nyuma ya Liverpool na moja mbele ya Southampton wanaokamata nafasi ya 7 huku Spurs ikikamata nafasi ya 6.

No comments

Powered by Blogger.