NITARUDI LIVERPOOL - LUIS SUAREZ

Mshambuliaji wa Barcelona ambaye jina lake litaendelea kubaki katika chati za klabu ya Liverpool Luis Suarez amesema kama atafikiria kurudi Kucheza nchini England basi itakua katika klabu ya Liverpool.

Suarez alikua kati ya nyota wengi wa Liverpool waliopamba mechi ya hisani iliyowakutanisha Steven Gerard akiwa na kikosi chake waliocheza dhidi ya Jamie Carragher aliyekua na kikosi chake.

Katika pambano hilo la kuchangisha pesa kwaajili ya mfuko wa Liverpool (Liverpool Foundation) timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 2-2. Team Gerard iliyokua na nyota kama Gerrard,Suarez na Torres ilipata magoli yote mawili kwa njia ya penati zilizofungwa na Steven Gerrard wakati Team Carragher ambayo ilikua na nyota kama Mario Ballotel na Didier Drogba ilipata mabao yake kupitia kwa Drogba na Ballotel.

Baada ya pambano hilo Suarez alionekana akifurahi muda wote na akafunguka na kusema kwasasa hafikirii kurudi England lakini katika soka lolote linawezekana na kama siku akirudi England basi atarudi kuichezea Liverpool.

+++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.