HALI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA HAIRIDHISHI
![]() |
| Vikosi vya Stars na Malawi wakati wanaimba nyimbo za Taifa |
Na Alex Sanga Mwanza
Hali ya Uwanja wa CCM Kirumba bado si nzuri hasa maeneo ya kuchezea (pitch) na unahitaji Marekebisho ya Hali ya Juu ili kuendana na changamoto zilizopo hasa swala la mvua.
Uwanja wa CCM Kirumba siku ya Jana ulikuwa umejaa Maji kutokana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha jijini hapa na kupelelea baadhi ya mashabiki wa Toto African kuingia na kuanza kutoa Maji kwa kuchota na kuweka kwenye Mabeseni ili kunusuru Mchezo mkubwa wa Soka kati ya timu ya Taifa ya Tanzania na Malawi ambao ulipigwa jioni ya siku ya jana.
Akizungumza na Wapenda Soka Meneja wa Uwanja huo John Tegete alithibitisha kuwa ni kweli uwanja wa CCM Kirumba ni Mbovu wakati ambao mvua hunyesha na kupelekea uwanja kujaa maji.
"Tatizo kubwa La Uwanja wetu hauna Mifereji ya kutolea Maji(drainage system)
Ile mifereji iliyopo imejaa matope na imeziba kabisa na haiwezi kutoa Maji" alisema Tegete
Uwanja wa Kirumba ulifanyiwa ukarabati wa baadhi ya sehemu hasa sehemu ya benchi la Ufundi la timu, sehemu za vyoo,upande wa VIP na Marefa.
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Malawi Young Chomodzi Baada ya Mechi ya jana alisikika akisema kuwa uwanja ni mbovu na ulikuwa umejaa Matope na kuwapa shida wachezaji wake wakati wa mechi
++++++++++++++++++++++++++

No comments