TANZANIA KUMPIGIA KURA BLATTER URAISI WA FIFA.


Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufikia Siku ya kupiga kura, kumchagua Rais wa Shirikisho la soka Duniani FIFA.

Maelezo ambayo yametolewa na Rais wa TFF  mheshimiwa Jamal Malinzi leo alipokua akiongea na Waandishi wa Habari ametanabaisha kuwa Tanzania itampigia kura Rais wa sasa Joseph Sepp Blatter ambaye anatetea nafasi hiyo.

Malinzi alifunguka zaidi na kusema kuwa kama ilivyo nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki itampigia kura Blatter baada ya makubaliano yaliyofanyika katika kikao cha FIFA mwaka jana wakati wa kombe la dunia kule Brazil ambapo  wajumbe wote toka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) walikubaliana kwa pamoja kwamba kura ya Uraisi wa FIFA watampa Sep Blater na hivyo TFF Wao kama wanachama wa CECAFA nao watampigia kura Blatter.

No comments

Powered by Blogger.