TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA IJUMAA
Hizi ndizo habari za uhamisho wa wachezaji ambazo zimezungumziwa sana siku ya Ijumaa
YAYA TOURE
Kocha wa Inter Milan Roberto Mancini amesema anatamani kumsajili kiungo wa Manchester City Yaya Toure mwenye miaka 31 baada ya kuonekana hakuna mwelekea kuhusu mkataba mpya.
(Sky Sports)
PABLO ALCACER:
Mshambuliaji wa Valencia Pablo Alcacer mwenye miaka 21 amesema ndoto yake ilikua kusaini mkataba mpya wa Valencia ambao ameusaini licha ya kutakiwa na Liverpool.
(Talksport)
KEVIN MIRALAS
Matumaini ya Tottenham Hottspurs kumsajili winga wa Everton Kevin Mirallas, 27 kabla ya kufungwa dirisha la usajili yanazidi kuongezeka na katika dili hilo atahusishwa pia Aaron Lenon ambaye ataenda Everton.
(Daily Mirror)
JUAN COADRADO
Dili la Chelsea kumsaini winga wa Fiorentina Juan Cuadrado, 26, linafikia katika hatua nzuri na atatangazwa rasmi muda wowote kama mchezaji wa Chelsea ambapo pia itamhusisha Andre Schurrle, 24, kwenda Wolfsburg akitokea Chelsea
(Daily Mail)
ENNER VALENCIA:
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho pia anataka kupeleka paundi milioni 21 kumsajili mshambuliaji wa West Ham Enner Valencia mwenye miaka 25.
(Sun )
SAMI KHEDIRA:
Klabu ya Trabzonspor imepewa nafasi kubwa kumsajili kiungo wa Real Madrid Sami Khedira mwenye miaka 27 ambaye pia anawaniwa na klabu nyingi za ligi kuu ya England.
.(Daily Star)
YOUNES KABOUL:
Tottenham hotspurs wako tayari kumtoa nahodha wake Younes Kaboul, 29, ambaye pia hucheza kama Beki wa kati ili kumpata mshambuliaji kinda wa Stuttgart Timo Werner mwenye miaka 18.
(Daily Mirror)
ANDERSON:
Mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester United na Internacional ya Brazil ili kusajiliwa kwa kiungo Anderson, 26, ambaye maisha yake katika klabu ya Manchester United hayaeleweki.
(Daily Telegraph)
DIEGO FORLAN
West Brom wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Diego Forlan, 35, kwa mkopo toka klabu ya Japan Cerezo Osaka.
(Express,Star, Wolverhampton)

No comments