BAYERN MUNICH YAANZA MWAKA KWA KICHAPO
Ligi kuu ya Ujermani maarufu kama Bundesliga imeanza raundi ya pili kwa mechi ya kwanza kupigwa mwaka huu wa 2015 baada ya kusimama kwa muda tangu mwezi wa 12 kupisha majira ya baridi yanayosababisha viwanja kujaa barafu.
Katika mechi hiyo ya kwanza mwaka huu mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo klabu ya Bayern Munich walikua ugenini katika dimba la Volkswagen Arena nyumbani kwa Wolfsburg na kuambulia kichapo cha bao 4-1.
Magoli ya Wolsfburg yalifungwa na wachezaji wawili tu mawili Bas Dost aliyefunga magoli mawili na Kevin De Bryne aliyefunga magoli mawili huku goli pekee la Bayern Munich likifungwa na Juan Bernat na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Ushindi wa bao 4-1 Wolfsburg.
Kwa ushindi huo Bayern Munich wanaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 45 huku Wolfsburg wakikamata nafasi ya pili na pointi zake 37.



No comments