FURAHA NA AMANI YA SIMBA IKO MIKONONI MWA JKT RUVU  



Kipigo toka kwa Mbeya City katikati ya wiki kilipelekea mafarakano ndani ya klabu ya Simba na kuleta majonzi miongoni mwa wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kongwe nchini Tanzania.


Simba inajitupa tena uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kupambana na JKT Ruvu timu ambayo huisumbua sana Simba na ushindi pekee leo ndiyo utakaoleta furaha kwa mashabiki na wapenzi pamoja na viongozi na wachezaji



Kocha Wa Simba Kopunovic alikaririwa akimkumbuka kiungo mshambuliaji wa Simba Saind Ndemla ambaye maumivu ya ya nyama ya paja yanazidi kumuweka nje ya uwanja katika pambano la Leo.

Itakua mtihani mwingine kwa kocha huyu ambaye ameanza vizuri kazi ndani ya Simba akichemka katika mechi mbili zilizopita na ushindi pekee utaisogeza Simba toka katika hatari ya kushuka daraja.



RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO


Simba vs JKT Ruvu

Coastal Union vs Mtibwa Sugar

Ruvu Shooting vs Stand United

Prisons vs Kagera Sugar

Polisi Morogoro vs Mbeya City

KESHO


Yanga Vs Ndanda FC

No comments

Powered by Blogger.