TETESI ZA USAJI WA WACHEZAJI BARANI ULAYA

Zikiwa zimebaki siku 12 kabla ya kufungwa dirisha la usajili barani Ulaya hizi ndizo habari ambazo zimetandanda katika mitandao mbali mbali leo:



MARQUINHOS:

Manchester United Wamekatishwa tamaa na klabu ya PSG baada ya kuambiwa kuwa beki raia wa Brazil Marquinhos mwenye miaka 20  ambaye United wanamtaka anapatikana kwa rekodi ya dunia paundi milioni 112
PSG walimnunua beki huyo kwa paundi milion 26 mwaka 2013 akitokea Roma.
 (Full story iko Sun)

KEVIN MIRALLAS:

Tottenham wanawania saini ya winga huyu kutoka Ubelgiji anayekipiga kayika klabu ya Everton na wako tayari kubadilishana na Aaron Lennon japokua Everton imekataa imekataa dili hilo
(Full story : Daily Mirror)

AXEL WITSEL

Kiungo wa Zenit St Petersburg  Axel Witsel mwenye miaka 26 ameonyesha njia Manchester United kumsajili baada ya kusema angependa kucheza katika Ligi kuu ya England huku Man United ikiwa ndiyo klabu iliyoonyesha kumwania.
(Full Story : Bleacher Report)

XAVI 

Kiungo wa Barcelona Xavi ameitaka klabu yake hiyo kumsainisha kiungo wa Arsenal raia wa Spain Santi Cazorla mwenye miaka 30.
(Full Story: Metro)

JUAN CUADRADO 

Chelsea wanataka kumsajili winga wa Fiorentina  Juan Cuadrado mwenye miaka 26, lakini watatakiwa kwanza kuwauza kwanza mshambuliaji wake raia wa Ujerumani Andre Schurrle mwenye miaka 24,  na winga Mohamed Salah
 (Full story: Daily Mirror)

JAMES MILNER

Kiungo huyu wa England anayekipiga katika klabu ya Manchester City anaweza kuondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu za Italia au Spain
( Full story : Guardian)

GABRIEL PAULISTA

Arsenal Wameanza mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Villareal mwenye miaka 24 Gabriel Paulista.
(Full Story : Telegraph)

STEPHANE MBIA

Crystal Palace wamejiandaa kumsajili nahodha wa Cameruni Stephane Mbia ambaye yuko huru kujiunga na klabu yoyote kwasasa.
 . (Full Story : Daily Mail)

No comments

Powered by Blogger.