MESSI AIPAISHA BARCELONA DHIDI YA ATLETICO MADRID.
Mechi ya kwanza ya kombe la Mfalme nchini Spain maarufu kama Copa Del Rey baina ya Barcelona na mabingwa wa Spain Atletico Madrid ilimalizika kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Staa wa mechi hiyo iliyoanza majira ya saa 6 Usiku alikua Lionel Messi aliyefunga bao pekee katika mechi hiyo kwa kumalizia mpira wa penati aliyopigwa na kipa Jan Oblak.
Barcelona waliwatumia wachezaji wake wote muhimu katika mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Nou Camp jijini Barcelona na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuingia nusu fainali kama watashinda au kutoka sare katika mechi ya marudiano kule Vicente Calderon jijini Madrid wiki ijayo.
××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments