SPURS YAHAHA KUPATA USHINDI NYUMBANI DHIDI YA SHEFFIELD UNITED
Sheffield United inayoshiriki ligi daraja la kwanza Nchini England maarufu kama Championship jana iliikomalia Totenham Hotspurs licha ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza kombe la Ligi maarufu kama Capital One.
Mchezo huo mkali uliopigwa jijini London katika uwanja wa White Hart Lane nyumbani kwa Spurs iliwabidi Spurs kusubiri mpaka dakika ya 73 kupata bao pekee tena likiwa la penati iliyofungwa na Andros Townsend.
Penati hiyo ilitokana na mchezaji wa Sheffield United Jay McEveley kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na refa wa mchezo huo Neil Swarbrick kuamuru ipigwe penati ambayo ilifungwa na Townsend.
Mtihani mkubwa kwa Kocha wa Spurs Pochettino itakua ni kujaribu kupata ushindi ugenini sasa katika mechi itakyopigwa wiki Ijayo huku Fainali za michuano hiyo zikipangwa kupigwa Wembley tarehe 1 mwezi Machi.

No comments