STRAIKA WA ARSENAL AJIUNGA NA CRYSTAL PALACE


Arsenal imeendelea kupeleka kwa mkopo washambuliaji wake baada ya kumpeleka Yaya Sanogo kucheza katika klabu ya Crystal Palace kwa mkataba wa mpaka mwisho wa msimu  wiki ilyopita pia Lucas Podoski alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Inter Milan ya Italia.



Mshambuliaji huyo ambaye huchezea pia timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21 anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Palace Allan Pardew ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea Newcastle United.

Sanogo mwenye miaka 21 ameanza katika michezo miwili tu ya Ligi akiwa na Arsenal tangu alipojiunga nayo mwaka 2013 toka Auxere ya Ufaransa

Atakumbukwa na Arsenal kwa goli lake alilofunga dhidi ya Borussia Dortmund mwezi Novemba mwaka jana katika ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Arsenal walishinda 2-0.

Alifunga ia magoli manne katika ushindi wa bao 5-0 walioupata Arsenal dhidi ya Benfica katika kombe la Emirates lakini ameshindwa kuonyesha makeke mbele ya Sanchez na Welbeck

No comments

Powered by Blogger.