KWA HAYA FIFA MMENIDANGANYA
Nilibahatika kumuona Thiery Henry niliwahi kujiita Ronaldinho namkumbuka Peter Schmeichel nimemshuhudia Xavi nilimpenda David Beckham, sikumfaidi Zizou vizuri.
Nawakumbuka kina Shevshenko ,Kaka wote walikua wakali, nachojivunia ni kitu kimoja tu , Kuwashuhudia Liones Mess na Cristiano Ronaldo wakifanya vitu ambavyo kabla ya uwepo wao vilikua ni vitu vya kufikirika tu , hakuna alie amini kwamba vinaweza kutokea , nachosikitika ni kwamba wamebadili maana halisi ya mpira wa miguu.
Wameibadili tuzo ya mchezaji bora wa dunia[ Ballon D'Or] kua tuzo ya mfungaji bora wa Madrid na Barcelona mbaya zaidi vichwa vya Wendawazimu vimepewa jukumu la kumchagua wanaetaka atwae tuzo na sio anaestahili kutwaa tuzo.
Leo hii anaetwaa tuzo ni aliefunga magoli mengi kuliko mwenzie na wala sio mchezaji bora, Nazikumbuka zama za kina Fabio Cannavaro Matthias Sammer,Michel Platini na wengine wengi najiuliza wangekuwepo uwanjani leo hii je wangepata hii tuzo? jibu ni hapana,
Ukiniuliza ni nini kilichomuweka David Luis kwenye kikosi bora cha dunia sina jibu na hata yeye hajui, Iniesta anafanya nini kwenye kikosi bora cha dunia ndio kabisa sielewi , Ukimuuliza Tony Kross ni nini kilichomuweka kwenye kikosi bora cha dunia hawezi kukujibu, Iniesta huyu sio wa kipindi kile , Davidi Luis; Kroos hawakua na namba za kudumu kwenye timu zao ( Chelsea & B Munich ) kabla ya kuhamia timu nyingine , Kombe la dunia Iniesta alirudi nyumban bado asubuh, David Luis licha ya kukosa namba Chelsea lakini pia aliliangusha taifa lake kombe la dunia , alikuwepo kwenye kikosi kilichofungwa 7, Je, waliyoyafanya ndani ya miezi hii minne ( august to December) ni bora kuliko waliyofanya wenzao ndani ya mwaka mzima?
Fifa wanazidi kunidanganya, Najiuliza tena , Kwanini Yaya Toure hayupo kwenye hiki kikosi? Nakuja kugundua bado ni kazi ya jopo la wendawazimu, Mchezaji bora wa bara la Africa , Club ya Manchester city na ligi ya Uingereza anakosa namba kikosi bora cha dunia?
Najiuliza , ni kigezo kipi kilichotumika kumpa tuzo ya goli bora James Rodriquez ? Kazi ya wendawazimu tena , waliamua kumpa tuzo walietaka ashinde dhidi ya aliestahili kushinda, Adidas na Nike wanaupeleka mpira wapi? Sioni sababu ya kuziita tuzo za mchezaji bora wakat wachezaji bora hawatunukwi , wanatunukwa wenye faida na Adidas au Nike , wanatunukwa wenye sura za Hollywood kwasababu za kibiashara ,
John Cruyff " Ballon D'Or? A bunch of journalists and people voting for their friends"
Mfumo ndio tatizo , ifike mahali mfumo ubadilike, mfumo uliopo wa kupiga kura unawakandamiza wanaostahili kupata tuzo, viwekwe vigezo na mashart atakae fit ndie mshindi, Ni kura hizi hizi zilitumika kumnyima tuzo Sneidjer 2010, kura hizi hizi zimemnyima Frank Ribery uchezaji bora wa dunia mwaka Jana , zimetumika kumnyima Manuel Neur haki yake mwaka huu , Kikosi bora cha dunia hakina mshambuliaji wa kati , kazi ya wendawazimu, Kikosi bora cha dunia kina washambuliaji wanne wa pembeni , wawil kulia wawili kushoto , tokea lini timu ikawa na four wingers? Nafasi ya Yaya Toure ndio iliibiwa hapa . Lakini utamlaumu nani? Kazi wamepewa wendawazimu
..... by Dan Pol

No comments