SIMBA HII BALAA YABEBA KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR


Kwa mara ya 3 Simba imeweza kubeba kombe la mapinduzi linaloandaliwa mjini Zanzibar kuadhimisha sherehe za mapinduzi ya Zanzibar ambayo kilele chake ilikua tarehe 12 Januari.



Simba imeshinda kwa penati 4-3 ikiifunga Mtibwa Sugar katika pambano ambalo lilimalizika kwa sare ya 0-0 ndani ya dakika 90

Timu zote zilicheza kwa tahadhari kubwa huku mtibwa wakishambulia kwa kushtukiza huku Simba wakipiga pasi nyingi na kushindwa kabisa kuipita ngome ya Mtibwa iliyokua ikiongozwa na mkongwe Shabani Nditi na mchezaji bora wa mashindano hayo Salim Mbonde

Simba ilikua ya kwanza kufunga penati baada ya Awadhi Juma kuanza kufunga na kisha Ally Lundenga kupiga penati ya kwanza kwa Mtibwa na kufunga.

Penati ya mwisho ya mtibwa ambayo ilipigwa na Vicent Barnabas ilidakwa kiufundi na kipa wa Simba Ivo Mapunda ambaye aliingia uwanjani dakika za majeruhi katika pambano hilo mahususi kwaajili ya mikwaju ya penati akichukua nafasi ya kipa chipukizi Peter Manyika Jr

++++++++++++++++++++++++++

MIKWAJU YA PENATI ILIKUA HIVI


● Simba
- Awadhi Juma - anapata

● Mtibwa
- Ally Lundenga - anapata

 ● Simba
- Shaaban Kisiga - Anakosa Said Mohamed anaokoa

● Mtibwa
- Shabani Nditi - Anapata

● Simba
- Hassan Kessy - Anafunga

● Mtibwa
- Ibrahim Rajab - Anakosa mpira unagonga mwamba

● Simba
- Hasan Isihaka - Anafunga

● Mtibwa
- Ramadhani Kichuya - Anapata

● Simba
- Dany Sserunkuma - Anapata

● Mtibwa
- Vicent Barnabas - Anakosa

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

SIMBA BINGWA


- Simba wamekua mabingwa kwa mara ya tatu baada kuchukua ubingwa huo mwaka 2008,2011 na 2015 na kuifanya kuwa bingwa mara nyingi wa michuano hiyo

+++++++++++++++++++++++++++++++

TUZO ZILIZOTOLEWA


  • Mchezaji bora - Salim Mbonde (Mtibwa)
  •  Kipa Bora - Said Mohamed (Mtibwa)
  • Mfungaji bora - Simon Msuva - 4 Goals (Yanga)

No comments

Powered by Blogger.