HATIMAYE ETO'O AJIUNGA RASMI NA SAMPDORIA
Mshambuliaji wa Everton Samuel Eto'o amejiunga rasmi na klabu ya Sampdoria ya Italia na kusa mkataba wa miaka mitatu na nusu utakaomweka klabuni hapo mpaka mwaka 2018.
Samuel Eto'o mwenyewe ameweka picha katika aksunti yake ya Twitter ikiwa na maneno "Vipimo vya afya vimekamilika na sasa niko tayari kwa changamoto mpya"
Nahodha huyo wa zamani wa Cameruni mwenye miaka 33 alijiunga na Everton kiwa mchezaji huru mwaka jana mwezi Agosti na kufunga magoli manne katika mechi 20 alizoichezea Everton katika mashindano yote.
Katika taarifa ya kocha wa Everton Roberto Martinez alimshukuru Eto'o kwa mchango wake alioutoa katika klabu hiyo hasa akiwa mhamasishaji mkubwa kwa vijana katika mechi za Ulaya na kumtakia mafanikio mema aendako.
Hii ni mara ya pili Eto'o anaenda Italia baada ya kujiunga na Inter Milan mwaka 2009 ambapo alifunga magoli 25katika miaka miwili aliyocheza Inter Milan.
msimu uliopita Eto's aliichezea Chelsea na katika mkataba wake wa mwaka mmoja ambapo alifunga magoli 12 katikamechi 35.

No comments