AUSTRALIA YATINGA FAINALI KOMBE LA MATAIFA YA ASIA
● Yaifunga UAE itakutana na Korea Kusini Jumamosi
Timu ya taifa ya Australia imeshinda bao 2-0 wakiifunga United Arab Emirates (Umoja wa Falme za Kiarabu) na kutinga katika fainali ya kombe la mataifa ya Asia kwa mara ya pili mfululizo.Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Newcastle lililojaa maji kutokana na mvua inayoendelea kunyesha Nchini Australia wenyeji Australia ambao ni waandaaji wa michuano hiyo mwaka huu walipata mabao yao mawili katika dakika 14 tu tangu mchezo ulipoanza mabao ambayo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Australia ilipoteza katika fainali ya michuano hiyo miaka minne iliyopita wakifungwa na Japan watatakiwa kukomaa na kubakiza kombe mwaka huu watakapoikabili Korea Kusini Katika Fainali ya mwaka Huu itakayopigwa katika jiji la Sydney Jumamosi hii.
Australia ilipata magoli yake kupitia kwa Trent Sainsbury dakika ya 3 badae Jason Davidson akiongeza la pili dakika ya 11 ikiwaacha UAE wakipoteza nafasi ya kufika fainali baada ya kufika Nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996.
Korea Kusini imeingia katika fainali katika mechi ya awali walipoifunga Iraq bao 2-0 katika mechi ya awali siku ya jana.

No comments