CHELSEA YADHIHIRISHA UMWAMBA WAKE KWA LIVERPOOL
Vinara wa ligi kuu nchini England klabu ya Chelsea jana usiku iliitupa njea Liverpool katika pambano kali la Nusu fainali ya pili ya Kombe la Ligi Capital One pambano lililopigwa katika dimba la Stamford Bridge jijini London.
Wakichagizwa na sare ya bao 1-1 waliyoipata katika mechi ya awali pale Anfield Chelsea walicheza kwa tahadhari kubwa huku Kipa Thibaut Coutois akiokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Liverpool wakiongozwa na Raheem Sterling.
Mpaka dakika 90 zinamalizika katika pambano hilo hakuna timu iliyoona lango la mwenzake ndipo zilipoongezwa dakika 30 kutokana na sheria zinazoongoza michuano hiyo na ndipo Mlinzi wa Chelsea Branslav Ivanoc alipowainua Mashabiki walioujaza uwanja wa Stamford Bridge
Mpaka mwisho wa Mchezo Chelsea waliibuka wababe baada ya kushinda kwa goli hilo moja na kupata ushindi wa jumla wa bao 2-1 ambao unawafanya kucheza fainali ya Tarehe 1 Machi ambapo wanamsubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya Sheffield United na Tottenham ambao katika mechi ya awali Tottenham walishinda bao 1-0 bao la Andros Townsend kwa penati



No comments