NDOTO YA CHELSEA KUTOFUNGWA MSIMU HUU YAISHIA KWA NEWCASTLE
Ile ndoto ya Chelsea kufikia rekodi iliyowekwa na Arsenal msimu wa mwaka 2003-2004 imepotea leo baada ya kuchapwa bao 2-1 na Newcastle United katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu nchini England katika uwanja wa Sports Direct maarufu kama St.James Park jijini Newcastle
Chelsea ambayo ilikua haijawahi kufungwa mechi yoyote msimu huu na wengi wakiamini pengine wangemaliza msimu huu bila kufungwa waliingia katika mchezo wa leo wakitaka kufikia rekodi iliyowekwa na Arsenal na Man United kwa kucheza michezo 15 mfululizo bila kufungwa.
Newcastle ambao walionekana wanajiamini na kucheza mipira mingi ya kustukiza iliwabidi kusubiri mpaka kipindi cha pili kujipatia mabao yake mawili yaliyofungwa na Papiss Cisse aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Remy Cabella magoli akifunga dakika za 57 na 79
Goli la Chelsea katika mchezo huo lilifungwa na Didier Drogba dakika ya 83 akiunganisha mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa kiufundi na Cesc Fabregas.
Newcastle United ilibidi wacheze pungufu kwa dakika zaidi ya 10 kabla ya mpira kuisha baada ya beki wake Steven Taylor kutolewa kwa kadi nyekundu ikiwa ni kadi ya pili ya njano alipomfanyia madhambi Eden Hazard.
Kwa matokeo hayo Chelsea wamepunguzwa kasi katika kilele cha ligi hiyo wakibaki na pointi zao 36 katika nafsi ya kwanza huku wakiombea Everton waifunge Manchester City badae ili tofauti ya pointi ibaki kuwa 6.
No comments