HABARI MBALIMBALI ZA SOKA KUTOKA LIGI KUU YA ENGLAND
- Kocha wa Newcastle, Alan pardew amesema anahofia kwamba Moussa Sissoko anaweza kuwa staa atayefuatia kuondoka klabuni hapo huku kukiwa na habari kwamba Chelsea na Arsenal wanainyatia saini ya kiungo huyo mfaransa.
- Golikipa wa everton Tim Howard ameibuka na shutuma kwa mkongwe Brad Friedal kwamba alijaribu kuzuia uhamisho wake kwenda Manchester United mwaka 2003. lakini golikipa huyo wa Tottenham amekana shutuma hizo.
- Wayne Rooney yupo tayari kucheza mchezo dhidi ya Southampton utakaopigwa siku ya jumatatu baada ya kukosa mchezo kati ya timu yake ya Manchester United dhidi ya Stoke.
- Kuna ripoti kwamba kocha wa Manchester United Louis Van Gaal anataka kumsajili beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne.
- Beki wa Stoke City Ryan Shawcros Amewaonya Arsenal kwamba wasitarajie mteremko watakapokutana Stoke leo katika uwanja wa Britannia.
- Kiongozi wa klabu ya MLS ya Marekani Don Garber Amesema wapo tayari kumruhusu kiungo wao City iwapo yeye mwenyewe taamua kufanya hivyo.
- Matajiri wa soka ulimwenguni, Real Madrid na Paris Saint-Germain wote wanamnyatia Eden Hazard lakini Chelsea wao wapo tayari kwa mazungumzo ya mkataba mpya.
- Porto wamesema mshambuliaji wao Mcolombia Jackson Martinez hauzwi pamoja na nia iliyooneshwa na vilabu mbalimali vya Uingereza zikiwemo Arsenal, Liverpool na Tottenham.
- Arsenal wanaandaa chambo nyingine ya Pauni milioni 15 kwa ajili ya kiungo wa Southamton Morgan Schneiderlin.
No comments