ARSENAL YAAMBULIA KICHAPO KWA STOKE
Juhudi za Arsenal kushinda mechi 3 mfululizo ziliishia mikononi mwa Stoke City ambao waliwapokea na kiustarabu kabisa wakawapiga bao 3-2 katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu England pambano lililopigwa katika dimba la Britania.
Dakika ya kwanza tu ya mchezo Peter Crouch anaipatia Stoke City bao la kwanza kufuatia makosa ya mabeki wa Arsenal kushindwa kuokoa mpira wa krosi.
Stoke walipata bao la pili na la tatu kipindi cha kwanza kupitia kwa Bojan Kirkic na Jonathan Walters na mpaka mapumziko Arsenal walikua nyuma kwa bao 3-0.
Kipindi cha pili Stoke City waliongeza bao la 4 ambalo Refa alikataa kwakua kipa alikua amezuiwa na Diouf wakati mfungaji Bojan akipiga. Arsenal wao walipata magoli yao mawili kupitia kwa Santi Carzola na Aaron Ramsey na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 3-2 Arsenal wakilala.
Mchezo uliopita Arsenal walishinda kwa bao 1-0 wakiifunga timu ngumu ya Southampton wakati Stoke walifungwa na Manchester United bao 2-1 na kwa matokeo ya leo Arsenal wanabaki na pointi zao 23 katika nafasi ya 5 wakati Stoke wao wamepanda mpaka nafasi ya 11 wakiwa na pointi 18.
No comments