MANCHESTER CITY YANOGESHA LIGI KUU ENGLAND.



Mabingwa watetezi Manchester City wamenogesha ligi kuu England baada ya kuifunga Everton kwa bao 1-0 na  kuisogelea kwa karibu Chelsea inayoongoza msimamovwa ligi hiyo.



Manchester City ambayo staa wake Sergio Aguero ilimbidi kutolewa dakika ya 5 tu ya mchezo baada ya kuumia ilipata bao lake pekee katika mchezo huo likifungwa na Yaya Toure kwa njia ya penati baada ya Jagielka kumwangusha James Milner eneo la hatari.

Tofauti ya pointi hivi sasa kati ya Vinara wa Ligi hiyo Chelsea na wanaokamata nafasi ya pili Manchester City ni pointi 3 hivyo kuzidi kunogesha ligi hiyo ambayo inakaribia kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.

Nafasi ya tatu na nne katika ligi pia inazidi kupendeza baada ya Manchester United wanaokamata nafasi ya 4 kuzidiwa pointi moja tu na Southampton wanaokamata nafasi ya 3 huku timu hizo zikitarajia kucheza mchezo wao wa ligi siku ya Jumatatu.

MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO

Newcastle United 2-1 Chelsea FC
Liverpool 0-0 Sunderland
Stoke City 3-2 Arsenal
QPR 2-0 Burnley
Tottenham. 0-0 Crystal Palace
Hull City 0-0 West Brom
Man City 1-0. Everton

No comments

Powered by Blogger.